Monday, November 26, 2007
Monday, October 29, 2007
Makamo wa rais Mstaafu Bw Suleiman Faida(L) Kassim Mrefu(C) na Gavana wa Blida(Atsa) Emson Shirima (R) wakifuatilia kwa makini moja ya hutba za Eid
Tuesday, October 16, 2007
Thursday, October 11, 2007
Wanafunzi wapya
Utaratibu kamili utatangazwa hapo baadae
CHAMA CHA WANAFUNZI WATANZANIA NCHINI ALGERIA
JINA NA HISTORIA YA CHAMA
a) Jina la chama ni : CHAMA CHA WANAFUNZI WATANZANIA NCHINI
b)Chama kiliundwa na wanafunzi Watanzania wasomao nchini Algeria ; Mwezi Aprili mwaka 2002 katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.
MLEZI WA CHAMA
Chama kina mlezi wake ambaye hupatikana kwa mapendekezo ya wanachama kwa wakati huo.
3.0. MALENGO YA CHAMA
Malengo na madhumuni makuu ya kuanzishwa chama ni pamoja na :
a)Kuwaunganisha wanafunzi Watanzania wote wasomao nchini Algeria katika kuwawezesha kuishi hali ya udugu, mshikamano na kujenga moyo thabiti wa kusaidiana na kushirikana.
b)Kubuni mbinu, mipango na mikakati mbalimbali na kuitekeleza kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya wanachama wake ili kupata maisha bora, na elimu iliyo nzuri.
AU
Kuandaa mazingira mazuri ya wanachama wake katika kuhakikisha wanapata maisha na elimu bora.
c)Kutafuta ufumbuzi, kushughulikia na kufuatilia matatizo makuu yanayowakabili wanachama wake hasa ya kiuchumi yanayotokana na gharama kubwa za kimaisha na kielimu.
d)Kutetea maslahi ya wanachama ikiwa ni pamoja na kusimamia kikamilifu na kuhakikisha wanapata haki zao zote kwa usawa na uadilifu bila upendeleo.
e)Kusimamia na kutekeleza kwa ujumla maazimio yote na maelekezo yatakayotolewa na wanachama.
f)Kudumisha uzalendo na kuendeleza uhusiano bora na jumuiya zingine za wanafunzi pamoja na mamlaka na ofisi mbalimbali hususani zile zinazoshughulikia masuala na matatizo ya wanafunzi.