Uongozi wa Atsa unapenda kuwataarifu wanachama wake kuwa unategemea kupokea ugeni kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali utakaokuja nchini Algeria kuanzia tarehe 01/11/2009 mpaka 06/11/2009.Lengo kuu la ziara hiyo itakayoongozwa na katibu mkuu wa wizara akiambatana na maofisa wanne wa wizara na mmoja kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ni kuangalia hali halisi na ni katika mazingira gani wanafunzi waTanzania nchini Algeria wanasoma,pia watapata fursa ya kuongea na wanafunzi na kusikia maoni yao pamoja na kusikiliza kero zao
Uongozi unawaomba wanafunzi wote wawe tayari kwa mapokezi ya ujumbe huo na inawakumbusha kuwa wahusika ndio watatuzi wa mambo yetu hivyo ni fursa pekee ya kuongea nao ana kwa ana na kuwaeleza kila kitu
Pia uongozi unapenda kuwajuulisha kuwa wanafunzi 58 wanaokuja kuanza masomo mwaka mpya wa masomo 2009/2010 watapelekwa katika mkoa wa Consantine na watasoma lugha ya kifaransa katika chuo kikuu cha Consatantine,siku na tarehe ya kuwasili Algeria bado haijajulikana
Uongozi unawatakia masomo mema na afya njema
Ahsanteni
UONGOZI
Saturday, September 26, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)